Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameahidi kuwapatia uwanja klabu ya Yanga eneo la Kigamboni Jijini Dar es salaam ambao watautumia kujenga kiwanja chao.

Ametoa ahadi hiyo jijini Dar es salaam katika harambee kubwa ya kuichangia klabu ya Yanga ijulikanayo kama ‘KUBWA KULIKO’ akisema kuwa ni kwa ajili ya kulipa deni la Rais mstaafu Jakaya Kikwete ambaye aliwahi kuchangia Sh. 30 milioni kwa ajili ya uwanja wa klabu ya Simba uliopo Bunju.

Amesema kuwa mchezo wa mpira wa miguu umekuwa ukichangia pakubwa pato la taifa, hivyo kuiwezesha klabu ya Yanga ni kuongeza njia nyingine ya uingizaji mapato

”Mimi niko hapa sio kama shabiki, lakini niko hapa kama serikali, katika kipindi cha Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete aliiwezesha Simba kupata uwanja, ilihali yeye anajua kabisa kuwa ni Yanga damu, hivyo basi na mimi nawapatia uwanja kule Kigamboni utakaowasaidia katika shughuli zenu za michezo,” amesema Makonda

Hata hivyo, Makonda ameongeza kuwa ameona nia ya dhati ya klabu ya Yanga kufufuka upya kwani mwenendo iliokuwa nao ulikuwa hauridhishi.

Omar al-Bashir kufikishwa kortini
Wakulima waiomba serikali kuwaongezea eneo la kilimo cha umwagiliaji