Wachezaji Harry Kane, Eden Hazard na N’Golo Kante wameongezwa kwenye orodha ya watakaowania tuzo ya Ballon d’Or baadae mwaka huu.

Ongezeko la wachezaji hao ni sehemu ya mpangilio uliowekwa na waratibu wa tuzo za Ballon d’Or, ambapo wanatangaza kwa utaratibu majina ya wachezaji hadi kufikia 30.

Wachezaji wengine waliotajwa mpaka sasa ni mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann pamoja na kiungo wa Real Madrid Isco.

Cristiano Ronaldo , Kevin De Bruyne na Roberto Firmino nao wametajwa katika awamu ya pili, ambayo iliwajumuisha wengine kama mlinda mlango wa Real Madrid Thibaut Courtois na beki wa Atletico Madrid Diego Godin.

Majina yaliyotajwa mpaka sasa ni:

 • Sergio Aguero (Manchester City)
 • Alisson (Liverpool)
 • Gareth Bale (Real Madrid)
 • Karim Benzema (Real Madrid)
 • Edinson Cavani (Paris Saint-Germain)
 • Thibaut Courtois (Real Madrid)
 • Cristiano Ronaldo (Juventus)
 • Kevin De Bruyne (Manchester City)
 • Roberto Firmino (Liverpool)
 • Diego Godin (Atletico Madrid)
 • Antoine Griezmann (Atletico Madrid)
 • Eden Hazard (Chelsea)
 • Isco (Real Madrid)
 • Harry Kane (Tottenham)
Shonza akerwa na watafuta kiki mtandaoni, Sister Fey atajwa
Mubarak Wakaso apata ajali

Comments

comments