Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteuwa Hawwah Ibrahim Mbaye kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Udhibiti wa Mfumo wa Utoaji wa Leseni za Biashara Zanzibar.

Mwinyi amefanya uteuzi huo hii leo Oktoba 5, 2022, ambapo kambla ya uteuzi huo Hawwah alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Leseni katika Baraza la Udhibiti wa Mifumo ya Utoaji wa Leseni Zanzibar.

Aidha, Rais Mwinyi pia amemteua Salmin Sharif Khatib kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar, na uteuzi huo umeanza rasmi hii leo Oktoba 5, 2022.

Puttin asaini sheria umiliki majimbo manne ya Ukraine
Museveni aomba radhi, ajitetea kumpandisha cheo mwanawe