Kundi la watu wenye silaha la Azawad ambalo lilitia saini mkataba wa amani mwaka 2015 nchini Mali, limetangaza kujiondoa kwenye mchakato wa kuandika rasimu ya katiba mpya, wakiulaumu uongozi wa kijeshi kutotilia mkazo mchakato wa kuwa na katiba mpya. 

Kundi hilo, linalounga mkono siasa za vuguvugu na linaloongozwa na jamii ya watu wa Tuareg, limetoa uamuzi wake huo baada ya kutia saini mkataba wa amani mwaka 2015 jijini Algiers nchini Agleria. 

Kikundi cha wapiganaji wenye silaha kikiwa kinakatika katika makazi ya raia nchini Mali. Picha ya Alliance.

Madai mengine yaliyoainishwa na kundi hilo ni kutokuwa na utashi wa kisiasa wa uongozi wa Jeshi, ili kuhakikisha kuwa mchakato huo unatekelezwa jambo linalotoa ishara kwa makundi mengine kuwa na uwezo wa kufikiria kujiondoa. 

Hata hivyo, wameomba mkutano na wasuluhishi wa Kimataifa ili kueleza changamoto wanazokabiliana nazo katika mchakato wa kupata amani ya kudumu na katiba mpya, wakati huu ambapo serikali ya kijeshi ikiahidi kukabidhi madaraka kwa raia mwezi Machi mwakani (2023). 

Ukosefu wa tiba HIV, Ukimwi wasababisha vifo maelfu ya Watoto
Uchunguzi waanza tuhuma wizi wa kura kwenye uchaguzi mkuu