Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Queens) imemaliza michezo ya hatua ya makundi ya michuano ya kombe la CECAFA Challenge inayoendelea mjini Jinja nchini Uganda, kwa kuambulia matokeo ya sare bila kufungana dhidi ya Ethiopia.

Kwa matokeo hayo, Kilimanjaro Queens itamenyana na wenyeji Uganda katika mchezo wa hatua ya nusu fainali uliopangwa kucheza siku ya Jumapili, huku mcheza mwingine wa hatua hiyo ukitarajiwa kuzikutanisha kati ya Kenya dhidi ya Ethiopia.

Mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya CECAFA Challenge kwa wanawake, umepangwa kufanyika Septemba 20, ukitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.

Video: Polisi Dar es salaam wakamata watuhumiwa ujambazi, mmoja mwanamke auawa
Malinzi Ampongeza Rais Mpya UEFA