Wenyeviti wa kamati mbili za bunge za hesabu za serikali PAC na ile ya serikali za mitaa LAAC, wamekosoa uamuzi wa baadhi ya Mawaziri waliojitokeza mbele ya waandishi wa habari na kuanza kupangua hoja za CAG kabla hazijafikishwa ndani ya bunge na kudai kitendo hicho ni cha udhalilishaji

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka na Vedasto Ngombale ambaye ni mwenyekiti wa LAAC, walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Aidha, Wenyeviti hao wamekosoa kitendo hicho mara baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Prof. Mussa Assad, kuwasilisha ripoti ya ukaguzi iliyoishia Juni 30, 2017 kwa waandishi wa habari mjini Dodoma wiki iliyopita kisha kuanza kuonekana kwa baadhi ya Mawaziri kujibu ripoti hiyo nje ya Bunge.

“Mawaziri sita ambao wamejibu hoja za CAG kupitia kwa waandishi wa habari wanakiuka sheria na hawapaswi kujibu badala yake wanaotakiwa kufanya hivyo ni makatibu wa wizara wenye wajibu ambao ndiyo wanaitwa na kuhojiwa na kamati husika,”wamesema wenyeviti hao

Hata hivyo, hii ni mara ya kwanza katika historia ya bunge, Mawaziri kujibu hoja zinazotolewa na CAG kabla hazijafikishwa mbele ya Wabunge.

Arturo Vidal kupigwa kisu
Manny Pacquiao amuweka mwalimu wake njia panda

Comments

comments