Wagonga nyundo wa jijini London (West Ham United), wameripotiwa kuwa katika mpango wa kumsajili kiungo kutoka nchini Hispania na klabu ya Chelsea Cesc Fabregas.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror, West Ham Utd wamejiandaa kuwasilisha ofa ya kumsajili kiungo huyo wakati wa majira ya baridi (Mwezi Janurui mwaka 2017).

Chelsea wanaamini suala la kuuzwa kwa Fabregas mwezi Januari mwaka 2017, litawapunguzia mzigo wa kumlipa mshahara wa Pauni 160,000 kwa juma, ambao kwa sasa anaendelea kuupokea bila kuvuja jasho.

Fabregas amekua na wakati mgumu wa kutimiza malengo ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea, chini ya utawala meneja Antonio Conte, hali ambayo imezua maswali mengi kuhusu mustakabali wa nahodha huyo wa zamani wa Arsenal.

Mbali na klabu ya West Ham Utd kutajwa, pia Fabregas anahusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na miamba ya soka mjini Milan nchini Italia AC Milan.

Ripoti ya tukio la Mwanafunzi kumuua mwalimu darasani yawekwa wazi
Video: Mtoto wa marehemu Samuel Sitta asimulia kifo cha baba yake