Wagonga nyundo wa jijini London West Ham United, wanajipanga kumsainisha mkataba mpya kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Dimitri Payet.

The Hammers wamedhamiria kufanya hivyo kutokana na fununu za kuondoka kwa kiungo huyo kushika kasi, huku klabu kadhaa zikihusishwa kuwa katika harakati za kukamilisha mpango huo.

Gazeti la The Sun limeripoti kuwa, Man Utd ni moja ya klabu zinazomuwania Payet, jambo ambalo limemshtua meneja Slaven Bilic ambaye siku zote amekua akimpigania kiungo huyo kubaki magharibi mwa jijini London.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hilo umebaini kuwa, West Ham United wamejipanga kumsainisha Payet mkataba ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni laki moja na ishirini na tano (125,000), huku mkataba wake wa sasa ukisaliwa na miezi tisa.

Klabu nyingine zinazotajwa kumuwania Payet mwenye umri wa miaka 29, ni mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG pamoja na mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid.

Virgil van Dijk Kuzipotezea Liverpool, Everton?
Ozil Atamani Kurudi Santiago Bernabeu