Wagonga nyundo wa jijini London (West Ham Utd) wapo katika hatua za mwisho za kumsajili mshambuliaji kinda kutoka nchini Argentina, Jonathan Calleri.

Gazeti la London Evening Standard limearifu kuwa, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atajiunga na West Ham Utd akitokea Boca Juniors, baada ya kupelekwa kwa mkopo nchini Brazil katika klabu ya Sao Paulo.

Meneja wa The Hammers, Slaven Bilic amemfuatilia kinda huyo kwa muda mrefu na kujiridhisha atamfaa kwenye kampeni za kusaka ubingwa wa England msimu wa 2016/17 ambapo West Ham Utd watautumia uwanja wa Olimpic kwa mara ya kwanza wakitokea Upton Park.

Hata hivyo taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinafafanua kwamba, pamoja na suala la usajili wa Jonathan Calleri kuwa kwenye hatua za mwisho, bado meneja huyo kutoka nchini Croatia ataendelea kusaka mchezaji mwingine katika nafasi ya ushambuliaji.

Mwenyekiti mwenza wa klabu ya West Ham Utd, David Sullivan aliwahi kuthibitisha mpango wa kusaka mshambuliaji ambaye atakuwa na uwezo wa kufunga mabao zaidi ya 20 kwa msimu.

Alisema tayari wameshatenga kiasi cha Pauni milion 30, kwa ajili ya kufanikisha mpango huo.

Antonio Conte: Soko La Usajili Limekua Na Changamoto Kubwa
Arsene Wenger Apata Majanga Arsenal