Wagonga nyundo wa jijini London, West Ham Utd wameanzisha tena mashambulizi ya kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Mexico pamoja na klabu ya Man Utd, Javier Hernandez Chicharito baada ya kusitisha mpango huo tangu mwezi uliopita.

West Ham Utd, waliamini usajili wa mshambuliaji huyo ungetosha kwa gharama ya paund milioni 8.5 ambazo waliziwasilisha sambamba na ofa waliyoituma Man Utd, lakini ombi lao liligonga mwamba na kutakiwa kuongeza dau.

Kwa sasa wameamsha mkakati wa kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, wakiwa na paund milioni 12, duru zinaeleza kuwa wamepanga kufanya ushawisi wa nguvu hadi wafanikiwe.

Suala lingine ambalo limewasukuma viongozi wa West Ham Utd, kuanzisha upya mchakato wa kufanya usajili wa Chicharito, limepewa msukumo na hatua ya kuumia kwa mshambuliaji kutoka nchini Ecuador, Enner Valencia ambaye atakua nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu.

Pia klabu hiyo ya magharibi mwa jijini London, inaendelea na mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya QPR Charlie Austin, lakini wanasisitiza mpango wa kutaka kupunguziwa ada ya usajili ambayo ilitajwa kuwa paund million 15, kutokana na mkataba wa mchezaji huyo unavyoelekeza.

 

Profesa Lipumba: Sina Mpango Wa Kujiuzulu CUF, Lakini…
Video: Alicia Keys na Swizz Beatz wapagawa na ngoma za Wizkid