Klabu ya West Ham iko mbioni kufikia makubaliano na kocha wa zamani wa Manchester City, Manuel Pellegrini kwa ajili yakuinoa klabu hiyo baada ya kuondoka kwa David Moyes.

Pellegrini mwenye umri wa miaka 64 ana uzoefu na ligi ya Uingereza kwani aliiwezesha Manchester City kutwaa ubingwa katika msimu wa mwaka 2013/2014.

West Ham watalazimika kutoa kiasi cha Paundi milioni 5 ili kumpata kocha huyo ambaye kwa sasa anainoa klabu ya Hebei China Fortune.

Wagonga nyundo hao wa London pia wamekuwa wakihusishwa na kumtaka Rafa Benitez ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Newcastle United na ameiwezesha Newcastle kumaliza msimu katika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

 

 

Juma Kaseja avuruga ya rekodi Simba
Makonda apokea msaada wa Mamilioni ya ujenzi wa Ofisi za walimu Dar