Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameitaka kamati ya Maadili ya Bunge kumpuuza mbunge wa Shinyanga mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Steven Masele kwa tuhuma za utovu wa nidhamu na kulidhalilisha bunge.

Amesema kuwa Masele amekuwa na tabia ya fitina na kuwachonganisha viongozi wa mihimili tofauti tofauti hivyo kusababisha kutokuwepo kwa maelewano kwa baadhi ya viongozi hao katika uwajibikaji.

”Kwakweli huyu Masele naiomba kamati ya maadili na bunge kwa ujumla tumpuuze Masele, maana anachokifanya ni uchonganishi tu, muacheni Rais afanye kazi, mna mzeesha bure Rais Magufuli kwa kumpelekea uongo na maneno yasiyokuwa na ukweli, wewe Masele mimi siwezi kukupa nyumba, VX wala usalama wa taifa wa kukulinda mpaka niambiwe na Raisi,”amesema Ndugai

Video: Kwa nini usitumie Diclofenac kutibu ugonjwa wa dengue?
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 24, 2019