Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amelielekeza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuanza msako wa kuwabaini Wezi wa Vifaa vya Magari, vibaka kuwakamata na kuwachukulia hatua Kali za kisheria.

RC Makalla ametoa maelezo hayo wakati wa Kikao Cha tathimini ya ziara yake ya kusikiliza Migogoro Jimbo kwa Jimbo ambapo amesema kumeanza kuibuka vitendo vya Wizi na kuleta taharuki kwa Wananchi jambo ambalo hawezi kulifumbia macho.

Aidha RC Makalla ametoa wito kwa wazazi kuchunguza mienendo ya watoto wao na kuwakanya ili wasijekuingia kwenye mikono ya Vyombo vya dola.

Agizo hilo limetolewa kwa mikono miwili na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Muliro Jumanne ambae amewaelekeza makamanda wote wa Mikoa ya kipolisi kuanza kazi ya kuwasaka wahalifu Mara moja.

Rais Samia apokea hati za utambulisho
Watoto 113 wakamatwa kwa uhalifu