Watu wasiojulikana wamevunja katika kitengo cha kuhifadhi vitu vya thamani vya mwimbaji Beyonce Knowles kilichoko Los Angeles Marekani na kuiba nguo, mabegi, pochi na vitu vingine vyenye thamani ya $1 milioni (sawa na Sh. 2.319 bilioni za Tanzania), kwa mujibu wa vyombo vya usalama.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 39 ana utajiri wenye thamani ya $500 milioni, kwa mujibu wa ‘Wealthgollira’ na ‘Forbes’.

Polisi wa Los Angeles wamewaambia waandishi wa habari kuwa katika tukio hilo vitengo vitatu vilivyokuwa vimekodiwa na kampuni ya Parkwood Entertainment Production inayomilikiwa na mwimbaji huyo, vilivamiwa mara mbili na wezi ndani ya mwezi huu.

Hata hivyo, vitendo vya wizi katika vitengo vya kuhifadhi vitu vya thamani vya watu maarufu vimeripotiwa mara kadhaa katika jiji hilo.

 Polisi wameeleza kuwa Januari mwaka huu, kitengo kinachomilikiwa na mwimbaji Miley Cyrus kilivamiwa. Wavamizi hao waliiba nguo, picha na vitu vingine vya thamani.

Mwaka 2018, Miley Cyrus aliwahi kupata pigo kama hilo baada ya vyumba vya hazina za vitu vyake vya thamani lilivamiwa huko San Fernando Valley, na wezi hao wakaondoka na gitaa lenye thamani kubwa ya fedha.

Kwa mujibu wa TMZ, hakuna mtu anayeshikiliwa na polisi hadi sasa kufuatia tukio la wizi wa mali za Beyonce ambaye ni mke wa rapa Jay Z.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 31, 2021
Whatsapp yakataa kila ujumbe kuwekewa alama