Mtandao wa kijamii wa WhatsApp maarufu kwa kutuma jumbe za sauti, video na maneno umeamua kuanza kufanya majaribio ya namna ya kuufanya mtandao huo kuwa wa usiri kama ilivyo mitandao mingine ya kijamii.

Kama ilivyo Instagram, Twitter, Facebook pamoja na mitandao mingine inayomlazimu mtu kuingiza taarifa zake za siri maarufu kama nywira (pasword), ili kuruhusu kufanya mawasiliano na kuperuzi vivyo hivyo wamiliki wa mtandao wa WhatsApp wameona umuhimu wa kuja na taarifa za siri za mtu binafsi ili kuweza kuutumia mtandao huo.

Tovuti ya kuaminika ya WABetaInfo wameeleza kuwa tayari yameanza majaribio ya kutumia alama za vidole kama nywira kufungua mtandao huo, ambao kila mtumiaji atalazimika kuufungua mtandao huo kwa kutumia alama za vidole vyake maarufu kama ‘Fingerprint’.

Zoezi hili litaanza ramsi kwa watumiaji wa simu aina ya Android.

Hata hivyo alama hizo za vidole zitaanza kutumiwa kuanzia kwenye ‘Home Page’ ya simu yako kwenye ‘Icon’ ya WhatsApp

Aidha, kwa kufanya hivyo itarahisisha kutunza taarifa binafsi za mtu hasa pale ambapo mtu amechukua simu yako au pale ambapo utakuwa umeibiwa simu yako.

'Kwanini tumsifie JPM wakati hizi ni kodi zetu?', Kakobe afunguka
LIVE: Rais Magufuli akipokea ndege nyingine ya Tanzania