Mtandao wa Kijamii wa WhatsApp umeweka zuio kwa watumiaji kutuma ujumbe mmoja mara tano tu, ili kukabiliana na kuenea kwa habari za uongo zinazo endeshwa kupitia mtandao huo.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Sera na Mawasiliano wa Kampuni ya WatsApp, Victoria Grand ambapo amesema kuwa sheria hiyo tayari ilishaanza kutumika nchini India tangu mwezi Julai mwaka jana .

Amesema kuwa sababu kubwa ya kuweka ukomo ni vifo vya watu vilivyotokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ambapo mwezi julai mwaka jana nchini India, vifo vya watu kadhaa vilitokea baada ya habari ya utekaji watoto kusambaa kupitia mtandao huo.

Aidha, nchini India habari za kuteka watoto zilienezwa na watu na kupelekea baadhi ya washukiwa wa utekaji kuuawa, kama mama mmoja ambaye alionekana akiwapa pipi watoto na familia yake walivamiwa na aliuawa na wanakijiji.

Pia Grand ameongeza kuwa kuanzishwa kwa mtandao huo kulilenga kuboresha mawasiliano ya watu binafsi huku akiongeza kuwa sheria hiyo itasaidia kufanya mtandao kufanya kazi iliyokusudiwa ambayo ni mawasiliano ya watu binafsi.

Katika mahojiano na gazeti la uingereza “The guardian”, mkuu wa kitengo cha mawasiliani WhatsApp, Carl Woog amesema kuwa wameamua kuweka ukomo wa kutuma ujumbe kwa watu watano au makundi matano kwasababu wana amini ni namba inayotosha kuwafikia ndugu wote na marafiki wa karibu na kuzuia matumizi mabaya ya mtandao.

Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita uongozi wa mtandao wa Facebook pia ulitangaza kufuta kurasa 500 na akaunti zinazojihusisha na usambazaji wa taarifa za uongo katika maeneo ya Ulaya ya kati, Ukraine, na nchi za Ulaya mashariki.

 

 

Uwindaji panya waharibu misitu
Mnangagwa arejea nyumbani, adai hali ni shwari