Shirika la Afya Duniani WHO limezindua mkakati mpya wa kupambana na kuiangamiza Saratani ya kizazi, kwa matumizi mapana ya chanjo, vipimo vipya na matibabu ili kuokoa maisha ya watu kufikia mwaka 2050.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, awali ilikuwa kama ndoto kupambana na kuondoa kabisa aina yoyote ya saratani lakini sasa shirika hilo limejihami na zana za gharama nafuu na za kutosha kukabiliana na Saratani.

Mkatati huo umetoa mwito kwa mataifa mbalimbali kutoa chanjo ya saratani ya kizazi angalau kwa asilimia 90 ya wasichana walio chini ya umri wa miaka 15 kufikia mwaka 2030.

Aidha WHO katika mkakati wake mpya imetoa wito kwa angalau asilimia 70 ya wanawake kuhakikisha wanapimwa saratani ya kizazi wanapofikisha umri wa miaka 35 na kisha kupima tena wanapofikia umri wa miaka 45 na angalau asilimia 90 ya waliopatikana na ugonjwa huo wanapokea matibabu.

Wanaofariki kwa kunywa sumu Kilimanjaro waongezeka
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 18, 2020