Mama waliojifungua wanashauriwa kusubiri kwa angalau muda wa mwaka mmoja ndiyo kushika ujauzito mwingine kwa ajili ya usalama wa afya yake na mtoto atakayejifungua.

Watafiti wameeleza kuwa ni vyema kusubiri kwa zaidi ya miezi 18, yaani mwaka mmoja na nusu kwa mujibu wa shirika la Afya la dunia.

Tofauti ya muda mchache kati ya mimba moja na nyingine inahatarisha maisha ya mzazi na kile kiumbe kinachotarajiwa kuzaliwa na mara nyingine husababisha mtoto kuzaliwa njiti.

Mtafiti, Dkt Wendy Norman amewashauri wanawake chini ya miaka 35 ambao wanafanya uzazi wa mpango kukaa kipindi cha muda huo ndio kushika mimba nyingine.

Amesema miezi 18 inatosha kwa mwanamke kufanya maamuzi ya kuzaa mtoto mwingine na kwa kiasi kidogo sana ana hatari ya kupata shida wakati wa kujifungua.

Taarifa hizi ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo kikuu cha British Columbia kwa kushirikiana na chuo cha Harvard TH Chan kinachojihusisha na mambo ya afya uliohusisha uzawa wa watoto 150,000.

Utafiti huo umeonesha kwamba miezi 12 hadi 18 ni miezi sahihi ya kushika ujauziti na kujifungua

Hivi karibuni Shirika la afya duniani limeongeza muda huo na kusema kuwa angalau miezi 24 sawa na miaka 2 au isiwe chini ya miezi 18.

Aidha utafiti huo umebainisha kuwa kupata mimba chini ya miezi 12 mara tu baada ya kujifungua ni hatari kwa mwanamke yeyote yule, lakini pia ni hatari zaidi kwa manamke mwenye umri zaidi ya miaka 35.

 

Video: Aina za wanaume wanaowavutia zaid wanawake
Makampuni 10 yatangaza nafasi za ajira, 'Apply hapa'