Shirika la Afya Duniani WHO, limetoa wito kwa Mataifa kuongeza juhudi za kupunguza vifo vitokanavyo na watu kuzama kwenye maji, huku likitoa mapendekezo sita ya kusaidia kupunguza vifo na ajali zinazosababishwa ajali za aina hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema sababu kubwa vya vifo hivyo hutokwna na watu kwenda kuteka maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, kuogelea, kusafiri kwa njia ya maji kwa kutumia boti na meli, uvuvi, athari za hali mbaya ya hewa na mafuriko.

Dkt. Tedros amesema, kauli mbiu ya siku ya kuzuia vifo vitokanavyo na maji kwa mwaka huu wa 2022 ni “Fanya jambo moja kuzuia kuzama” inayotumika katika siku hiyo ya Kimataifa kuzuia vifo ulimwenguni kwa watoto na vijana wenye umri wa kati ya mwaka 1 mpaka miaka 24.

Usafirishaji wa idadi kubwa ya watu na mizigo kuliko uwezo wa chombo unaohatarisha maisha.

Taarifa ya Mkuu huyo wa WHO, iliyotolewa Geneva Uswisi hii leo Julai 25, 2022 imeeleza kuzama kunasababisha vifo vya zaidi ya watu 236,000 kila mwaka na asilimia 90 ya vifo hivyo vikitokea katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati huku watoto walio chini ya umria wa miaka mitano wakiwa katika hatari kubwa zaidi.

Hata hivyo, Dkt. Tedros ameeleza kuwa “Vifo hivi vinaweza kuzuilika kupitia kutafuta suluhu za msingi zenye ushahidi n aza gharama ya chini. Leo miji na majiji mengi ulimwenguni yatawasha taa yenye mwanga wa rangi ya bluu kuandishiria wito wa kuchukua hatua za kuzuia na kukomesha watu kuzama.”

Rais ajaye atakiwa kuzijali kaya masikini
SADC yawahimiza Waandishi matumizi Kiswahili