Shirika la Afya Duniani (WHO), limetangaza hali ya hatari kufuatia kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa wa ZIKA unaosababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Margaret Chan ameeleza kuwa tahadhali zaidi zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya ugonjwa huo sawa na ile iliyotolewa kwa ugonjwa wa Ebola.

Dk Margaret Chan

Dk Margareth Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Alisema kuwa utafiti na kipaumbele zaidi kwa kujikinga zinapaswa kutolewa kuwalinda wanawake wajawazito na watoto duniani kote dhidi ya virusi hivyo vilivyosababisha maelfu ya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo.

Hata hivyo, kwa upande wa Afrika Mashariki bado hakujaripotiwa kesi inayohusu maambukizi ya virusi vya ZIKA yanayatokana na mbu aina ya Aedes wanapowauma wanawake wajawazito. Mbu hao huuma majira ya mchana.

WHO imewataka wanawake wajawazito kuhakikisha wanajikinga na mbu kwa kupaka au kupuliza dawa za kufukuza mbu.

Uchaguzi Marekani: Ted Cruz amshinda Donald Trump Mchujo wa jimbo la Lowa
Tanzia: Diwani wa CUF AUAWA KWA MAPANGA