Kiungo mshambuliaji Georginio Gregion Emile Wijnaldum yupo shakani kucheza mchezo wa mwanzoni mwa juma lijalo ambapo klabu yake ya Liverpool itakua mwenyeji wa Man Utd katika uwanja wa Anfiled.

Wijnaldum ameibua hofu ya kuukosa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengu duniani, kufuatia majeraha aliyoyapata wakati wa mchezo wa kuwania kucheza fainali za kombe la dunia kati ya timu yake ya taifa ya Uholanzi dhidi ya Ufaransa uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo mjini Amsterdam.

Kiungo huyo ambaye alisajiliwa na Liverpool akitokea Newcastle miezi mitatu iliyopita, alilazimika kutolewa uwanjani, baada ya kulalamika anahisi maumivu makali sehemu za nyuma ya paja.

Georginio Wijnaldum holds his hamstring as he limps out of Holland's clash with France in AmsterdamGeorginio Wijnaldum akitoka uwanjani baada ya kupata majeraha ya paja.

Tayari meneja wa Liverpool Jurgen Klopp  ameagiza mchezaji huyo kufanyiwa vipimo ili kufahamu kama atakuwa na uwezo wa kumchezesha katika mchezo ujao wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Man Utd.

Tangu aliposajiliwa huko Anfield, Wijnaldum ameshacheza michezo 11, na kabla ya kujiunga na timu yake ya taifa alikua sehemu ya kikosi cha Liverpool kilichoibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Swansea City.

TFF Yashindilia Msumari Wa BMT, Yashindwa Kuitambua Yanga Yetu
Juuko Aungana Na Wenzake Jijini Mbeya