Kila mwananchi anahitaji kuwa na afya bora, siyo yule tu wenye kipato cha juu na kumsahau mwenye kipato cha chini ndio maana serikali ya awamu ya tano kupitia viongozi mbalimbali wanahitaji kuweka usawa katika Sekta zote.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happi anadhihirisha hilo kuhakikisha ya kwamba wananchi hawapati usumbufu wanapokwenda katika vituo vya afya vya wilaya ya kinondoni kwa kutatua kero za gharama za  ambazo zinakuwa haziandikiwi risiti.

Amesema mfumo wa kulipa dirishani ni miradi ya kutengeneza pesa ambao unawashirikisha watu wa maabara na wale wahasibu madirishani kwa kutotoa risiti kitu ambacho Mganga Mfawidhi hakifahamu ndio maana amefikiria mfumo wa kadi

Aidha ameongeza kuwa Wilaya ya kinondoni itakuwa ya kwanza kutumia mfumo wa kisasa wa kutumia  kadi kulipia matibabu na kusema kuwa kwa miezi 12  kadi hiyo itakuwa na kiasi cha Elfu 40  huku lengo likiwa ni kudhibiti ufujaji wa mali.

Kadi hizo ambazo ziko chini ya manispaa zinatarajiwa kuanza kutumika kuanzia July 25 2016.

Majaliwa afungua Maadhimisho ya Sita Wiki ya Maji Afrika
Raisi Magufuli;Wafanyakazi Wa jeshi la Polisi Wasiokua Askari Wahamishiwe Utumishi