Bondia Deontay Wilder ambaye hajawahi kuonja kipigo, akishinda mapambano yake yote 39 huku akiwazima wapinzani wake kwa KO mara 38, amesema kuwa anaamini Bingwa wa Dunia wa Mashumbwi ya Uzito wa Juu, Anthony Joshua anamuogopa, lakini amemtia moyo.

Wilder amedai kuwa ingawa amepanga kumpasua Joshua kwenye pambano lao litakalofanyika mwakani, anaamini haitakuwa mwisho wake wa kuendelea na mchezo huo kwani bado ni kijana mdogo anayeweza kujipanga upya.

“Nataka pambano hilo lifanyike mapema iwezekanavyo. Nadhani ananiogopa, sitaki kusema kuwa yeye ni muoga. Lakini nadhani anahofu juu yangu,” Wilder aliiambia TMZ.

Hata hivyo, pambano kati ya wawili hao linaonekana kuwa na changamoto ya mgao wa kifedha kati ya wababe hao.

Wilder anataka mgao uwe nusu kwa nusu (50-50) kwakuwa yeye bado ni bingwa wa dunia wa WBC. Promota wa Joshua, Eddie Hearn anapambana mteja wake apate mgao mnono zaidi kwakuwa anashikila mikanda ya ubingwa wa IBF na WBA.

Wilder anaamini kuwa yeye ndiye bondia anayeogopwa zaidi na mwenye heshima zaidi kwenye ulimwengu wa masumbwi ya uzito wa juu kwa sasa kutokana na jinsi alivyowazima wapinzani wake ulingoni.

Joshua ameshapanda ulingoni mara 20 na kushinda mapambano yake yote kwa KO (Knock Out). Hivyo, wote ni mabingwa ambao hawajawahi kupoteza pambano.

Mawakili wa Kenyatta kutinga mahakamani kesho
Video: Nyalandu aanza kazi Chadema, Maajabu ya 'tajiri' aliyetaka kununua mahekalu za Lugumi