Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Crystal Palace, Dazet Wilfried Zaha, amesema hana mpango wa kuikacha klabu hiyo wakati wa dirisha la usajili, na badala yake ataendelea kuwa sehemu ya kiksoi msimu ujao.

Mshambuliaji huyo alieamua kuitumikia timu ya taifa ya Ivory Coast mwaka 2017, licha ya kuzaliwa katika kitongoji cha Croydon nchini Uingereza, amesema ni wakati mzuri wa kuendelea kuwa na Crystal Palace ambayo anaamini inamtosha.

Zaha alijaribu kucheza soka nje ya klabu hiyo, baada ya kusajiliwa na Man Utd 2013, lakini alikutana na changamoto kubwa ya kuwania nafasi katika kikosi cha kwanza na hatimae alirejea tena Selhurst Park mwaka 2015.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, tayari anahushishwa na mipango ya kusajiliwa na mabingwa wa soka England Manchester City, kwa ada ya Pauni milioni 50.

“Sina mpango wowote wa kuondoka,” amesema Zaha.

“Ninafurahia maisha ya soka nikiwa Crystal Palace, naamini hata wewe unaona namna ninavyofurahia mazingira ya hapa.” Aliongeza Zaha kumwambia mwandishi wa habari wa Sky Sports

Zaha amefanikiwa kufunga mabao tisa katika ligi ya England msimu wa 2017/18 uliofikiatamati jana Jumapili, na ametoa mchango mkubwa wa kuifikisha Crystal Palace katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi.

Alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi April na tayari ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa klabu ya Crystal Palace.

Nondo ataja sababu tatu za kumtema wakili wake
Tanzania yatinga fainali kombe la dunia