Mustakabali wa kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil Willian kuendelea kubaki ama kuondoka Chelsea, bado haueleweki kutokana na pande hizo mbili kushindwa kufikia makubalino hadi sasa.

Taarifa zinaeleza kuwa Willian anahitaji mkataba wa miaka mitatu ili abaki klabuni hapo, tofauti na hapo amesisitiza ataondoka na kwenda kucheza soka mahala pengine ambapo wataonyesha wanamthamini. Chelsea wamempatia ofa ya mkataba wa miaka miwili pekee na hivyo utofauti wa mwaka mmoja ndio changamoto.

Willian ambaye ameweka wazi adhima yake ya kuendelea kubaki jijini England, bado hajaweka wazi kama atakubaliana na mkataba aliopewa na Chelsea au ataamua kujiunga na timu zingine zilizopo England.

Klabu za Totenham na Arsenal zote z jijini London zinahusishwa kwenye mpango wa kumuwania kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye anaaminiwa ataweza kuongeza ladha kwenye moja ya vikosi vya klabu hizo.

Hata hivyo wakala wa Willian – Kia Joorabchian amenukuliwa akisema ” Sidhani kama Willian amebadilika kwa namna yeyote. Amekuwa mtulivu muda wote. Tulipokua ofa kubwa kutoka Marekani – MLS ambayo ilimtaka ajiunge nao Julai Mosi – lakini amekuwa akihitaji kumaliza msimu na Chelsea na kisha atafanya maamuzi siku moja baada ya mchezo wao wa mwisho”

 “Ana ofa mbili kubwa kutoka Ligi Kuu Uingereza – EPL, MLS na mbili za Ulaya . Ataamua baada ya mchezo wa mwisho”

Chelsea wanaonekana kutosumbuka katika hili kwani wamefanya mabadiliko katika sera yao ya mikataba kwa wachezaji wenye umri wa zaidi ya miaka 30. Mwanzoni walikuwa wanaongeza mwaka mmoja na sasa wanaongeza miaka miwili, hawaonekani wakijiongeza zaidi kufikia miaka mitatu kwa wachezaji wenye umri huo.

Lampard alinukuliwa akisema “Naelewa hali ilivyo kwa upande wa klabu. Nina mahusiano mazuri na Willian lakini sijui maamuzi ni yapi. Kama yatatokea wiki ijayo muda wowote kama anavyosema Willian], basi ni sawa kwa upande wangu vyovyote vile.”

“Nina furaha sana na Willian, amekuwa na mchango mkubwa kwangu na timu kwa ujumla. Utendaji kazi wake na morali kwenye timu ni kitu kikubwa kwangu na timu kwa msimu huu”

“Ni maamuzi yake na nina yaheshimu. Kama akiamua kuondoka , basi Chelsea pia itapaswa kuendelea kutafuta mshambuliaji mwingine”

Chelsea wameshasajili washambuliaji wawili ambao wanaweza kucheza katika nafasi ya Willian. Tayari wamemsajili Timo Werner na Hakim Ziyech, sasa hivi wanapambana kuitafuta saini ya kinda Kai Havertz.

Konde Boy aahidi makubwa Simba SC
Man Utd wana mlima wa kupanda UEFA Europa League