Wananchi nchini Uganda wameingiwa na hofu kubwa mara baada ya wimbi la utekaji kushamili nchini humo, ambapo mpaka sasa watu 24 hawajulikani walipo.

Kwa mujibu wa Gazeti la Monitor nchini humo limesema kuwa kikundi cha polisi kinachofanya uchunguzi kimesema kuwa watuhumiwa 27 wamekamatwa na wengi 17 wamefunguliwa mashtaka mahakamani.

Aidha, Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo, Emilian Kayima amesema kuwa utekaji huo unaongezeka kila siku huku akitaja sababu kubwa ikiwa ni masuala ya biashara na wivu wa kimapenzi.

“Vitendo vya utekaji vimeongezeka nchini kwetu, vitendo hivi vinasababishwa na makubaliano ya kibiashara, pia wivu wa mapenzi, tunawashauri watu wote kuripoti polisi pindi wakiona ndugu yao hajaonekana ndani saa 24,”amesema Kayima

Hata hivyo, Kayima amewaasa wananchi wa nchi hiyo kutoa taarifa sahihi ya maeneo husika wanayopendelea kutembea au wanapokutana na jamaa zao ili kurahisisha kufanyika kwa uchunguzi pindi linapotokea tatizo.

Hatma ya 'Sugu' kujulikana leo
Askari watumia risasi za moto kwa waandamanaji, waua