Rapa Azma Mponda amesema kuwa wimbo wake mpya alioubatiza jina la ‘Garagasha’ anaoamini ni ‘hit’ ijayo, umeingia mtaani kimakosa bila idhini yake.

Wimbo huo ambao Dar24 imeupata kutoka kwa chanzo chake, umewakutanisha Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi, Mtoto wa Mbeya Izzo Bizness pamoja na mrembo Abela.

“Ni kweli nimekamilisha project yangu hiyo ambayo nimewashirikisha Sugu, Izzo na Abela, lakini nasikitika kuona umeingia mtaani hata kabla sijauachia rasmi. Unajua nimewahi kuwapa watu wangu wa karibu sana kuusikiliza na kuutolea maoni kama ambavyo wasanii tumekuwa tunafanya, so nadhani kuna kitu hakikwenda sawa katika hilo,” Azma ameiambia Dar24.

Akizungumzia mpango wa kuiachia rasmi ‘Garagasha’, Azma amesema kuwa ameamua kuachia wimbo huo rasmi hivi karibuni ikiwezekana wiki hii ikiwa ni pamoja na video yake.

Azma anafanya vizuri hivi sasa na wimbo wake ‘Astaravaste’ aliomshirikisha Belle 9.

Endelea kufuatilia Dar24 tutaweka wimbo uliorasmishwa.

Video: Prof. Mkumbo ateuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara Maji
Kinyago Champonza Emerick Aubameyang