Mbunge wa jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu amemtaka Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kupeleka majibu bungeni kumweleza sababu za kufungiwa kwa wimbo wa ‘Mwanaume mashine’

Ameyasema hayo wakati akiahirisha kikao cha bunge ambapo amemtaka Waziri, Dkt. Mwakyembe kupeleka sababu za kufungiwa kwa wimbo huo kwa kuwa yeye anaona ni wimbo ambao hauna mapungufu na ndani ya wimbo huo wamezungumziwa wa kina Kichuya na kina Tabwe ambao ni wachezaji wa Simba na Yanga.

“Waziri kwenye majibu hebu nielimishe kidogo kuhusu huu wimbo ‘Mwanaume mashine’ umeufungia kisa nini, maana wimbo huu unamtaja Kichuya, Msuva na Jumapili tunataka tuisikie hebu tuambieni sababu ya kuifungia ni nini,”amesema Zungu

Video: Magufuli acharuka, Kikwete aungana na Mkapa janga la elimu
Polisi, Mahakama zakumbwa na kashfa nzito ya rushwa