Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo ameishauri Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kuona namna ya kuanzisha shule mpya ili kuleta uwiano wa waalimu katika shule hizo unaoendana na idadi ya wanafunzi ambao wanatarajiwa kuongezeka kila mwaka mpya wa masomo.

Wangabo amesema hayo wakati aliposhiriki kwenye ujenzi wa madarasa nane ya Shule ya Sekondari Kirando yanayotarajiwa kutumiwa na wanafunzi 422 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 katika shule hiyo inayobeba wanafunzi kutoka katika kata mbili zilizopo wilayani Nkasi.

“tunapoangalia kutatua changamoto ya shule hii ya Kirando Sekondari tuangalie ufumbuzi wa kudumu zaidi, muangalie uwezekano wa kujenga shule nyingine, huo ndio utakuwa ufumbuzi, shule hii ina O – level na A – level, sasa kama kutakuwa na shule nyingine ya O – level peke yake na hii mkaipunguzia mzigo wa kuchukua wanafunzi wengi na walimu wengi katika shule moja”

Pia, ametoa rai kuwa kwa eneo la ekari 60 linalomilikiwa na shule hiyo ya Sekondari Kirando inawezekana kugawa walau ekari 20 kwa shule hiyo mpya jambo litakalowapelekea kupewa waalimu wapya kwa shule mpya na kuleta uwiano wa waalimu kuliko hali ilivyo sasa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mtanda aliyapokea maagizo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kuanzia ngazi ya Kijiji hadi ngazi ya halmashauri ya Wilaya na kuongeza kuwa suala hilo litawekwa katika bajeti ya mwaka 2018/2019 na kuongeza kuwa wananfunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza watasioma.

“Wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha kwanza katika shule hii ya Kirando ni 422 na tumekubaliana kuwa hadi kufungua shule wananfunzi wote hao wanatakiwa wawe madarasani, lakini tumekubaliana na wazazi kuwa kama serikali tutanunua meza zote 422, lakini tumewahamasisha kuchangia walau mchango wa kiti ili mwanafunzi anapokuja akute meza na kiti ili tulimalize jambo hilo,”

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari kirando Erneo Mgina wakati akitoa taarifa fupi ya shule hiyo amesema kuwa shule ina wanafunzi 677 na kutaraji kupokea wanafunzi 422 na upungufu wa madara nane ambayo matatu tayari na mengine yapo katika hatua ya msingi na kutaraji kurekebisha vyumba vitatu vya maabara ili kuwahifadhi wanafunzi kwa muda hadi madarasa yatakapokamilika.

Hili limekuja ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI kuitaka mikoa iliyokuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 ukiwemo mkoa wa Rukwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata madarasa ya kusomea, madawati na vyoo pale shule zitakapofunguliwa tarehe 8/1/2018

Jela kwa kuoa mama na binti yake
Video: Tundu Lissu achambuliwa, NEC yazijibu hoja za Ukawa