Wakati mwaka ukielekea ukingoni, sakata la kupotea kwa Faru John limegubikwa na wingu zito baaada ya baadhi ya vigogo wa Wizara ya Maliasili na Utalii kushindwa kutoa majibu sahihi zaidi ya kujikanganya  kwenye maelezo yao, ambapo hali hiyo imezidi kuibua maswali  bila majibu ingawa tayari Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameunda tume ya kuchunguza utata wa faru John.

Wakati Tume hiyo ikiendelea na uchunguzi, baadhi ya vigogo wa Wizara hiyo walizungumzia kifo cha faru huyo huku wakishindwa kueleza faru huyo alikufa lini na kwa ugonjwa gani na wapi alipelekwa.

Aidha, kwa upande wake Mkurugenzi Masaidizi wa Uendelezaji wa Wanyama Pori, Dk. Nebbo Mwina na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Dk. Idd Mfunda walitoa ufafanuzi kuhusu faru John huku wakitofautiana na kushindwa  kutoa majibu sahihi.

Hata hivyo walisema kuwa Faru huyo badala ya kuhamishiwa kwenye hifadhi nyingine ya taifa alipelekwa kwa mtu biafsi (Grumeti) huku Dk. Mwina akisema alipelekwa Grumeti akazalishe faru wengine kwani huko kulikuwa na faru jike, na kuongeza kuwa Grumeti ni wadau wao wakubwa kwa sababu walikuwa wanaleta faru kutoka uingereza.

Wakati Dk. Mwina akitoa maelezo hayo, Dk. Mfunda amesema pembe hizo zina biashara, lakini haifanyiki Tanzania bali wanaojihusisha nayo ni wafanyabiashara haramu. pia amesema kuwa pembe za Faru John zilishakabidhiwa kwa Waziri Mkuu na kutoa maelekezo, na kwamba hata baada ya kifo cha faru pembe hizo zilichukuliwa na kuhifadhiwa.

 

 

Video: Lema azidi kunasa, Serikali yakata mikopo wanaosoma ng'ambo...
Bodi ya mikopo kuwasaka wadaiwa nyumba kwa nyumba, kwenye sherehe