Winnie Madikizela Mandela, aliyekuwa mke wa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ameishukia serikali ya nchi hiyo kuwa imeiingiza nchi kwenye janga.

Akizungumza na BBC katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Mandela, alisema kuwa nchi hiyo imefanya kosa kubwa kwani chama tawala cha ANC ‘kinaharibu’.

“Kuna kitu hakiko sawa kabisa kutokana na kile tulichokifanya katika maamuzi yetu,” BBC inamkariri.

Kauli ya Mama Winnie inakuja wakati ambapo kumekuwa na shinikizo la kumuondoa madarakani Rais Jacob Zuma kutokana na kashfa kubwa za matumizi mabaya ya madaraka zinazomkabili.

Rais Zuma anakubwa na kashfa ya kujihusisha na familia tajiri ya Gupta ambayo imedaiwa kuwa na uwezo wa kuingilia teuzi mbalimbali za viongozi pamoja na maamuzi yanayofanywa na serikali.

Mwaka 2014, ndege binafsi ya familia ya Gupta ilitua katika uwanja wa ndege wa jeshi la Afrika Kusini, hali iliyozua gumzo ambapo Rais Zuma alihusishwa pia na tukio hilo.

Rais Zuma anatarajia kuachia ngazi ya uongozi wa ANC mwishoni mwaka huu lakini muhula wake wa urais utakoma mwaka 2019. Bunge la nchi hiyo lilipiga kura ya kuamua hatima yake ya uongozi lakini kura za kumkubali zilitosha.

Video: CCM walivyomlilia mke wa Dkt. Mwakyembe
Video: Serikali yaionya Chadema, DC amweka ndani Nagu