Familia ya mpiganaji na mjasiriamali maarufu Duniani Floyd Mayweather inapitia kipindi kigumu zaidi kufuatia kesi nzito inayoendelea kumkabili mtoto wa Familia hiyo aitwaye Yaya Mayweather ambaye alishtakiwa kwa kumchoma kisu mpenzi wa zamani wa mwanaume aliyenaye kwenye mahusiano rapa NBA Young Boy.

Kwa mujibu wa OutKick, Taarifa za awali zinasema binti huyo anaweza hukumiwa kifungo cha hadi miaka 20 gerezani kwa kosa hilo.

Vurugu hizo zilitokea mwezi April mnamo mwaka 2020 ambapo Yaya ambaye ana mtoto mmoja na NBA YoungBoy, alijikuta kwenye vita nzito ya maneno na Mwanamke huyo aitwaye Lapattra Jacobs mpaka kupelekea kumchoma Kisu na kumjeruhi vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa Yaya Mayweather alifanikiwa kupata mtoto mapema mwezi Januari 2021.

NBA YoungBoy alikamatwa na polisi mapema mwezi March, baada ya kukimbizana na polisi dakika kadhaa akijaribu kutoroka.

Hukumu ya kesi ya Yaya Mayweather itasomwa mwezi Februari mwaka 2022.

Rais Ndayishimiye apokelewa na mwenyeji wake
Tanzania yapaa viwango vya soka duniani