Mwanamke mmoja anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mumewe kwa kumchoma shingoni na kitu chenye ncha kali mara baada ya mwanamke huyo kupokea simu ya mumewe iliyopigwa na mwanamke mwingine.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika katika hospitali ya rufaa kwa uchunguzi zaidi.

Tukio hilo limetokea siku ya jumatano mnamo saa mbili na nusu usiku katika mkoa wa Shinyanga, kitongoji cha Malenge kijiji cha Jomu kata ya Tinde.

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, Simon Haule amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo yaliyofanywa na Zena Mohamed mwenye umri wa miaka 28 ambapo ameelezea chanzo cha mauaji hayo kuwa ni wivu wa mapenzi baada ya mke ambaye ni Zena kupokea simu ya mume wake Bakari Saleh iliyokuwa ikiita na kisha kusikia sauti ya mwanamke mwingine  na kuhisi kuwa ni mchepuko.

Kufuatiwa tukio hilo Zena Mohamed aliamua kuchukua sheria mkononi kumuadhibu kwa kumchoma na kitu chenye ncha  kali, ndipo mauti yalipomfika mumewe Bakari Salehe mwenye umri wa miaka 35.

Aidha kamanda Haule ametoa wito kwa wananchi kuachana na vitendo vya dhana ya wivu wa kufikra.

Amesema ” Tuache kufikiri kuwa mwanaume akiongea na mwanamke au mwanaamke akiongea na mwanaume kwa njia ya simu au njia ya kawaida lazima kuna mahusiano  ya kimapenzi, jambo ambalo si kweli hasa kutokana na masuala ya utandawazi katika dunia hii ya leo”.

Mwanachuo akamatwa kwa kumiliki bastola
TCRA yawafunda wamiliki wa mitandao ya kijamii