Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekabidhiwa rasmi hospitali ya rufaa ya mkoa Maweni iliyopo mkoani Kigoma.

Akikabidhiwa hospitali hiyo Katibu Mkuu wa wizara hiyo dkt. Zainab Chaula amesema kuwa anashukuru sekretarieti ya mkoa kwa kuisimamia hospitali hiyo pamoja na watumishi katika kipindi hicho na hivyo kuwezesha wananchi kupata huduma zinazostahili.

“Pamoja na makadhibiano tutaendelea kushirikiana kwa ukaribu na ofisi yako RAS na bado utaendelea kuwasimamia watumishi hawa kwani wapo mkoani kwako”. amesema dkt. Chaula

TMA: Hali ya hewa hairuhusu nzige kutua Tanzania

Amebainisha kuwa wizara yake wametengeneza mkataba na RAS katika eneo la usimamizi hasa ya majengo ili yaweze kubaki kwenye uimara unaohitajika.

ametoa ahadi kuwa “Tunawashukuru watendaji wa ofisi ya katibu tawala kwa kazi nzuri waliyoifanya ya usimamizi wa hospitali hiyo hadi sasa tunakabidhiana, tutakwenda kuzisoma nyaraka hizi moja baada ya nyingine, maana ni mali za Serikali, mmetueleza kuna madeni tutayapitia na kuyafanyia kazi,”

Naye Katibu Tawala wa mkoa wa kigoma, Rashid Machatta alisema bado ataendelea kushirikiana kwa ukaribu na watumishi wa hospitali hiyo katika utekelezaji wa majukumu yao ili wananchi waweze kupata huduma bora.

Corona yaathiri utalii nchini

“ Watumishi sisi bado ni wamoja, tutashirikiana bega kwa bega ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma zilizo bora”. Amesema  Machatta.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo dkt. Osmond Dyegula amesema hospitali hiyo ina jumla ya watumishi 233, kwa wastani wanaona wagonjwa kati ya 300 hadi 330 kwa siku.

Wizara ya afya imekabidhiwa hospitali hiyo ikiwa ni agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuhamishia usimamizi huo wizara ya afya mwaka 2017 kutoka chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

NEC: Hatujatangaza ratiba ya uchaguzi mkuu
TMA: Hali ya hewa hairuhusu nzige kutua Tanzania