Wizara ya Afya nchini Uganda, imesema maambukizi ya Ebola yameongezeka katika Wilaya zote nchini Uganda, na kufanya idadi ya vifo vilivyothibitishwa na kushukiwa hadi sasa kufikia 23 na kwamba hakuna kesi yoyote iliyogunduliwa katika mji mkuu wa Kampala.

Uganda, ilitangaza mlipuko wa Ebola Jumanne iliyopita (Septemba 20, 2022), baada ya kisa cha ugonjwa huo nadra kugunduliwa katika wilaya ya Mubende iliyopo kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala.

Virusi vya ugonjwa huo, tayari vimeenea katika wilaya jirani za Kyegegwa na Kassanda, huku Wizara ya Afya ikiripoti kuwa visa zaidi vimeongezeka na kufikia 36, ikiwa ni pamoja na kesi zilizothibitishwa na zinazohisiwa.

Wizara hiyo imesema, “Inayowezekana kuambukizwa kama mtu yeyote ambaye alikufa kutokana na EVD inayoshukiwa (ebola), na alikuwa na kiungo cha janga la kisa kilichothibitishwa lakini hakupimwa na hakuwa na uthibitisho wa maabara na watu walikuwa pamoja naye.

Hata hivyo, Wizara inasisitiza kwa kusema, “kesi zilizothibitishwa kama zile zilizo na matokeo chanya ya maabara kati ya idadi ya maambukizo yaliyotambuliwa hadi sasa, ni 18 na zimethibitishwa kuambukiza na wengine 18 wakishukiwa kuwa na virusi hivyo.”

Aidha, Wizara ya Afya inasema, wagonjwa watano kati ya waliokufa walithibitishwa kufariki kutokana na virusi hivyo, huku 18 kati yao wakiorodheshwa katika vifo vinavyowezekana na takriban wagonjwa 35 wamelazwa mpaka kwa sasa.

Waziri Mkuu ashiriki mazishi ya Shizo Abe
Wataka mkataba wa amani, ongezeko la ghasia