Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Idara Ustawi wa Jamii imetembelea familia zilizoathirika na mauaji ya watoto na kutoa msaada wa kisaikolojia.

Akizungumza katika ziara hiyo Kiongozi wa Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hanifa Selengu amesema kuwa Wizara imeamua kujumuika na wanafamilia hao kwa kuwapa msaada wa kisaikolojia na kijamii ili kuondokana na msongo wa mawazo.

“Tumeguswa sana na msiba huu na matukio ya mauaji yaliyotokea na kwa niaba ya Wizara tunawapa pole kutokana na majanga haya na tuko pamoja kuhakikisha mnapata msaada muhimu ya kisaikoloji na kijamii,”amesema Selengu

Naye Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Rehema Kombe amesema kuwa msaada wa kisaikolojia na kijamii ni muhimu sana kwa familia zilizokumbwa na matatizo hayo ya mauaji ya watoto kwani familia zimekumbwa na taharuki kubwa.

Kwa upande wake , Gorden Mfugale aliyepoteza mtoto wake Gidrack Mfugale (5) amewashukuru wataalam hao kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Idara Ustawi wa Jamii na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wameona umuhimu wa kuwasaidia ili kuomdokana na msongo wa mawazo.

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Idara Ustawi wa Jamii ipo mkoani Njombe kwa kushirikiana na Wataalam wa Mkoa huo katika jitihada ya kutoa msaada wa Kisaikolojia na kijamii kwa familia zilizoathirika na matukio ya mauaji ya watoto mkoani Njombe.

Mavunde asheherekea Valentine's Day kwa kutoa misaada
Video ya mwanamke anayejinyoa vinyweleo kwenye ‘bodaboda’ yatikisa