Wizara ya Afya imemtuma Mtaalamu Bingwa wa uchunguzi (Pathologist) kutoka hospitali ya Rufaa Bugando mkoani Mwanza leo Agosti 30, 2018 kwa ajili ya kwenda kuchunguza upya mwili wa mtoto Sperius Eradius ambaye amefariki dunia siku chache zilizopita kufuatia adhabu ya kupigwa shuleni.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kupitia akaunti yake rasmi ya mtandao wa Twitter na kusema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mtoto huyo na kuongezea kuwa tayari mtaalamu huyo ameshawasili mkoani Kagera kwa ajili ya uchunguzi huo.

Awali uchunguzi wa mwili wa marehemu ulifanywa katika hospitali ya Rufaa ya mkoani Kagera lakini wazazi wa marehemu wamesema kuwa hawana imani na uchunguzi huo na hivyo kuiomba Serikali iweze kufanya utaratibu mwingine wa uchunguzi zaidi.

”Kufuatia wazazi wa mtoto kutokuwa na imani na uchunguzi uliofanywa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera, Wizara yangu imetuma mtaalamu bingwa wa uchunguzi Pathologist toka hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando kwa ajili ya kwenda kufanya uchunguzi wa mwili wa marehemu” ameandika Ummy kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Aidha ametoa wito kwa familia, ndugu na wananchi kuwa watulivu  katika kipindi hiki ambapoi uchunguzi wa kibingwa unaendelea amesema atahakikisha uchunguzi unafanyioka kwa ufanisi ili haki iweze kutendeka.

 

 

Jaji Mkuu wa Tanzania awapa neno wanasheria wa serikali
Maisha yava vitu 7