Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Elimu ya Afya Kwa Umma kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mpimbwe wameanza uelimishaji umuhimu wa Chanjo ya Surua kwenye mikusanyiko ya watu  kwa kutumia  ubunifu wa Kabila la Asili la Kisukuma.

Hatua hiyo itahakikisha kila jamii inafikiwa  na Ujumbe kupitia Minada na lugha ya Kabila la Asili la Kisukuma ikitumika juu ya uelimishaji hasa wananchi wakiaswa  kuacha dhana potofu kuwa mtoto mwenye Surua amelogwa na badala yake wawapeleke vituo vya kutolea huduma za Afya pindi waonapo dalili za ugonjwa.

Kupitia sanaa watahakikisha wanafikisha ujumbe kwa lugha inayozungumzwa katika eneo hilo kwani kuna baadhi ya watu hawajui lugha ya Kiswahili na pamekuwa na dhana potofu kuwa mtoto akiumwa amelogwa hali ambayo husababisha watoto wengi kupelekwa kwa Waganga wa Tiba Asili lakini wanapozidiwa ndipo hufanya maamuzi ya kuwapeleka Vituo vya kutolea huduma za Afya wakiwa wamechelewa.

Msanii wa nyimbo za Asili Majimoto, Winga Ititi.

Ugonjwa wa Surua, husababishwa na Virusi na huambukiza rika lolote lakini huathiri zaidi watoto na moja ya dalili zake ni kukohoa, koo kuuma, madoa ya rangi ya Kijivu  na nyeupe sehemu ya ndani ya mashavu, upele mwekundu na macho kuwa mekundu.

Baada ya kuripotiwa visa vya Ugonjwa wa Surua katika Mkoa wa Katavi, Wizara ya Afya imeshatuma timu ya wataalam Kwa ajili Elimu ya uhamasishaji Chanjo ya Surua huku Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akianza Ziara Leo  Februari 23.2023 na siku ya Ijumaa Februari 24.2023 atafanya Mkutano na wananchi katika Kijiji cha Mkuyuni  kata ya Majimoto  Halmashauri ya Mpimbwe  wilaya ya Mlele mkoani Katavi .

Kuhusu takwimu za  hali ya Ugonjwa wa Surua nchini, jumla wagonjwa wote waliothibitika kuwa na maambukizi ya Surua ni 667 kwa kipindi cha Julai ,2022 hadi Februari 2023 huku vifo 12  vikiripotiwa katika Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele ambapo asilimia 59 ya wagonjwa waliothibitika  kuwa na Maambukizi ya Surua  hawakuwa wamepata chanjo.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 24, 2023
Ubaguzi wa Rais waamsha hisia za watetezi haki za binadamu