Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, imekanusha taarifa zilizozagaa kuhusu kutenguliwa kwa agizo la Dkt. Harison Mwakyembe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kuhusu uchambuzi wa habari za magazeti katika redio na televisheni kuwa ni za uzushi.

Aidha, taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas imesema kuwa taarifa zilizozagaa hazina ukweli wowote na Rais Dkt. John Magufuli hajazungumzia chochote kuhusu agizo hilo la Waziri wa habari Dkt. Harison Mwakyembe.

“Tunapenda kuutaarifu umma kuwa taarifa hizo ni za uongo na uzushi uliotungwa kwa dhamira ovu kwani Rais hajatoa tamko, maagizo wala maelekezo yoyote yenye nia njema yaliyotolewa na Dkt. Mwakyembe,”amesema Dkt. Abbas.

Vilevie Dkt. Abbas amesema kuwa Umma unakumbushwa kuwa kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mitandaoni, 2015 kinakataza na kutoa adhabu kali ikiwemo kifungo jela kwa wanaoeneza taarifa za uongo.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa mitandao ya kijamii inatakiwa kutumika vizuri ili kuweza kupeleka ujumbe uliojitoshereza kwa jamii na uzushi.

Magazeti ya Tanzania leo Mei 5, 2017
Zifahamu Mbinu Chafu Na Sababu Za Rafiki Msaliti Kumchukua Mpenzi Wako