Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa wapo katika mchakato wa kufungua kituo cha huduma kwa wateja ‘Customer Service Center’ kitakachowasaidia wakulima kuwasilisha changamoto zao mbalimbali.

Bashe amebainisha hayo leo Februari 2, 2021 Jijini Dodoma katika Mkutano wa Pili wa Bunge la 12, wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo amesema kuwa wapo katika hatua za mwisho ya huduma hiyo ambayo itakuwa msaada kwa wakulima.

“Tupo katika hatua za mwisho kuanzisha kitu kinaitwa ‘Customer Service Center’ ambapo mkulima popote alipo nchini ataweza kupiga simu bure pale atakapopata pembejeo feki au kupata tatizo la kiatilifu au ugonjwa katika Wilaya yake ili aweze kuhudumiwa kwa wakati,” amesema Bashe.

Aidha Bashe amewahimiza wakulima kuhakikisha wanapata risiti ya EFD ya muuzaji pindi wanapoenda kununua pembejeo, ili mkulima atakapopatwa na tatizo serikali iweze kumchukulia hatua mhusika.

Himid Mao atua Entag El-Harby SC
Uganda: Jeshi lakemea ujumbe wa vitisho ulioenea mitandaoni