Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku kumi na tano kwa Wizara ya madini kupitia na kufanya marekebisho ya kanuni za uuzaji na uchakataji wa madini ya Tanzanite.

Ametoa agizo hilo wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha pamoja Cha Tanzanite Magufuli (Magufuli Tanzanite One Stop Center) kilichopo Mirerani Mkoani Manyara.

Majaliwa amesema kuwa kurekebishwa kwa kanuni ya biashara ya madini ya Tanzanite itasaidia kujenga heshima ya nchi kupitia eneo la Mirerani ambalo linazalisha madini hayo.

Hata hivyo ametoa miezi mitatu kwa wachakataji, wauzaji na wanunuzi wa madini ya Tanzanite nchini kufanya mpango wa kujipatia maeneo nakujenga ofisi zao eneo la Mgodi huo kama sehemu ya kuitangaza nchi kwa mataifa mengine.

Young Africans yalamba dili zito
Safari ya Kigoma, Manara kumpambania Mzee Mpili