SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imepanga
kuboresha na kuimarisha vivutio vya utalii wa ndani ikiwemo
fukwe na bahari na huduma za hoteli za kitalii nchini
ilikuhakikisha kuwa Wizara hiyo inavuka lengo la ukusanyaji
mapato.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani wakati wa mkutano
na waandishi wa habari akizungumzia fursa na mchango wa sekta
ya utalii katika kukuza uchumi wa taifa.

Alisema lengo la uboreshaji wa huduma hizo ni kufikia
utekelezaji na wa Mipango ya Sekta ya Maliasili na Utalii
katika kuchangia kuongezeka kwa pato la taifa na
hatimaye kukuza uchumi wa nchi.

“kuna haja ya kuboresha, kuongeza  nguvu na kuimarisha kila
hitaji ili kuwezesha sekta ya Maliasili na Utalii kuzalisha
zaidi ili kuchangia pato la taifa na hatimaye kukuza uchumi
wa Taifa “ alifafanua Mhandisi Makani.

Pia alisema kuwa Wizarainalenga kuboresha utangazaji wa
vivutio, bidhaa, na huduma, kuboresha miundo mbinu ndani ya
hifadhi, kuhifadhi vivutio na mazingira yake, kuboresha
utoaji wa huduma pamoja na kuendeleza vivutio vilivyopo na
kuanzisha vivutio vipya.

Gondwe Aunguruma Handeni,Apiga Marufuku Kucheza Bao Na Pool Table Wakati Wa Kazi
Jaji Lubuva Akabidhi Ripoti Ya Uchaguzi Kwa Spika Wa Bunge Job Ndugai