Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa imepanga kufanya matembezi maalum kwa ajili ya kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoa wa Kagera.

Wizara hiyo imeshirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, kuandaa matembezi ya Kilometa 5, yakianzia ‘Police Officer’s Mess’ iliyoko Osterbay/Masaki jijini Dar es Salaam, Septemba 17 mwaka huu kuanzia saa 12 asubuhi.

Washiriki wanatakiwa kuchangia kiasi cha shilingi 10,000 ya ushiriki wao, huku watu wote wenye mapenzi mema na wenye uwezo wakiombwa kuchangia kupitia akaunti maalum ya Benki iliyotolewa.

 

Imethibitishwa: Mabaki yaliyookotwa Pemba ni ya Ndege ya Malaysia iliyopotea
Wananchi wamkubali JPM, Twaweza watoa matokeo utafiti 'Rais wa Watu?....'