Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imejibu ombi la Baraza la Diaspora la Watanzania duniani (Tanzania Global Diaspora Council- TGDC) la kutaka vitambulisho vya taifa vitolewe na Ofisi za Ubalozi ili kupunguza gharama kwa Diaspora.

Katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Tagie Daisy Mwakawago katika balozi zote za Tanzania nchi mbalimbali imesema kuwa imepokea mrejesho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuhusu maombi ya Diaspora.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na NIDA, utaratibu wa kusajili na kutoa vitambulisho vya Taifa kwa Diaspora bado unafanyika nchini kupitia dawati maalum ambalo liko chini ya Bi. Rose Joseph kwenye ofisi ya NIDA iliyopo Ukonga- Mombasa jijini Dar es salaam.

Hata hivyo, taarifa hiyo imezitaka balozi zote katika nchi mbalimbali duniani kote kusambaza taarifa hiyo kwa Diaspora wote katika maeneo yao.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 7, 2018
Mwigulu Nchemba afunguka kuhusu milioni 50 za kila kijiji