Ikiwa tayari ndege ya Ethiopia Airlines imeanza kufanya safari zake katika mkoa wa Mwanza kwa ajiri ya kubeba minofu ya  samaki inayovuliwa katika ziwa victoria, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya ametembelea kiwanda cha Tanzania Fish Processors Ltd kinachojihususha na kuchakata samaki kilichopo mkoa wa Mwanza.

Baada ya kujionea shughuli nzima ya uchakataji wa samaki Manyanya ameelekeza viwanda vyote vya samaki nchini vinavyosafirisha minofu ya samaki kwenda nje ya nchi kuhakikisha vifungashio vyote vinawekewa alama au maelezo ya kuonesha  bidhaa hizo zinatoka Tanzania (Made in Tanzania)  kabla ya kutoka nje ya Viwanda au kwenye mipaka ya Tanzania.

Ziara ya Mhandisi Stella Manyanya ilikuwa na lengo la kujionea uzaliahaji unaofanywa na viwanda  vya samaki pia kujua changamoto wanazozipitia katika hatua za kuchakata samaki ambao watakuwa wanasafirishwa na ndege ya Ethiopia Airline kwenda katika nchi mbalimbali.

Akitoa taarifa Mkurugenzi wa rasilimali watu wa kiwanda cha Tanzania Fish Processors Ltd Bw. Goodfray Samwel amemushukuru Rais Magufuli kwa kuwa na maono ya kufanya Tanzania kuwa ya nchi yenye uchumi wa viwanda pia akampongeza kwa kuendelea kuweka sera nzuri Zenye malengo ya kuendeleza viwanda pia kufufua viwanda vingine ambavyo vilikuwa havifanyi kazi.

Naye Naibu waziri Wa Viwanda na Biashara ametoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya tano ili kuboresha viwanda vyote nchini hasa viwanda vya samaki ambazo zina soko kubwa katika nchi mbalimbali kote duniani.

“Serikali imejipanga kuhakikisha inaboresha sekta ya uvuvi ambayo ni sekta muhimu katika kukuza uchumi  kutoka na umuhimu wake wa uhitaji wa malighafi ya samaki ambazo zinasaidia viwanda vya samaki kote nchini kuendelea kufanya kazi na kukua kwa kasi” Ameeleza Manyanya

Na kuongeza kuwa “kutoka na changamoto nilizozisikia Serikali imejipanga kuanzisha taasisi mbalimbali za utafiti wa samaki katika ziwa victoria, pia tumejipanga kuanzisha masoko ya samaki, sambamba na hayo Tutakuwa na utaratibu wa kukutana mara kwa mara kati ya serikali na vyama vya wafanyabiashara wa samaki ambayo itasaidia kutatua kero mbalimbali ambazo wafanyabiashara wanakabiliana nazo’’

Katavi: Mtuhumiwa ubakaji auawa kwa fimbo
Waziri Mkuu azindua Kigoma ya mawese, kugawa mbegu bure