Ili kuongeza pato la Taifa na kuinua uchumi wa mkulima mmoja mmoja Wizara ya Kilimo imekutana na wadau na wakulima wa chai kujadili namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zitakazofanikisha kuinua kiwango cha zao hilo nchini.

Akizungumza hii leo Novemba 14, 2019 jijini Dodoma Naibu Waziri wa Kilimo Husein Bashe amesema kikao hicho kinatokana na kuanguka kwa sekta ya kilimo cha chai na kwamba lengo lao ni kuwa na kauli moja baada ya kuainisha changamoto za kilimo cha zao hilo itakayowasogeza kwenye mafanikio.

“Wadau hawa tumekutana nao na wametoka sehemu mbalimbali na pia wapo Wizara ya fedha kwa pamoja tunataka kuona ni namna gani tunaweza kuondoa changamoto zilizopo katika sekta ya kilimo cha chai na kuibuka na kauli moja ya mapambano,” amefafanua Bashe.

Ajali za maji: TEMESA kutoa elimu kwa watumia vivuko

Amesema kukutana kwao pia kunatokana na zao hilo kukumbwa na changamoto za aina mbalimbali zinazoikabili sekta ya hiyo kwani kwa miaka kumi sasa sekta ya kilimo cha chai inakuwa kwa asilimia moja pekee hivyo juhudi za pamoja zinahitajika ili kuokoa zao hilo.

“Tayari tumeunda timu inayoshirikisha Serikali, sekta binafsi na taasisi zitakazo simamia zao la chai na tumetengeneza mpango mkakati wa miaka mitano ambao utasimamia ukuaji wa kilimo cha chai ili itoke kwenye uzalishaji wa chai tani 37,000 na kufikia tani laki moja,” amebainisha Naibu Waziri Bashe.

Aidha amesema katika kujadiliana zimeibuka changamoto mbalimbali ikiwepo suala la kodi za mamlaka ya mapato nchini (TRA) kwa viwanda vya usindikaji chai na kwamba tayari wamekubaliana na Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato kukutana na kuona ni jinsi gani wanatatua kero hiyo.

Changamoto nyingine ni pamoja na kutokuwa na sehemu ya pamoja ya kukusanyia mazao yao kwa ajili ya usafirishaji ikiwepo uaandaaji wa vibali vya pamoja sambamba na mpango wa kuanzishwa kwa mnada wa zao la chai Jijini Dar es saalam.

Aidha amebainisha kuwa ipo haja ya kufanyia mabadiliko baadhi ya sheria, na wanatarajia kuanza kulifanyia kazi suala hilo katika mwaka ujao wa fedha na kuongeza kuwa suala la watu kutolipwa kwa wakati nalo ni changamoto na ameagiza wakulima walipwe ndani ya siku 15 kwa mujibu wa taratibu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa usimamizi bodi ya chai Tanzania Kemerina Kafanabo amesema chanzo cha kuharibika kwa chai itokayo mashambani kabla ya kufika kiwandani inatokana na ubovu wa miondombinu na kwamba kupitia kikao hicho wataona ni namna gani ya kuondokana na tatizo hilo.

Amesema ipo haja ya kuongeza upatikanaji wa pembejeo na kuiomba serikali kuongeza wataalamu wa kilimo katika maeneo hayo ili kuongeza ubora wa chai inayozalishwa viwandani.

Majaliwa aitahadharisha jamii madhara ya ulaji usiofaa
Video: Mkapa arusha kombora kwa Wabunge, wasomi, Ni Spika vs Chadema