Mapigano ya kikabila, yaliyosababishwa na wizi wa Pikipiki katika eneo la Darfur nchini Sudan, yamesababisha vifo vya karibu watu 24 na kupelekea hali ya dharura katika eneo hilo kutangazwa.

Kiongozi mmoja wa kikabila, Souleyman Abir amesema mapigano hayo yamesababisha uharibifu, nyumba kuteketezwa, mali kuporwa na kudai kuwa hali bado ni tete licha ya maafisa wa usalama wa serikali kuwasili eneo hilo.

Pikipiki ya mmoja wa Watalii katika Jangwa la Sahara. Picha ya Francois Steyn.

Mamlaka za Usalama, Viongozi wa Kisiasa na Kidini nchini humo licha ya kuziomba pande zinqzohusika katika mapigano hayo kusitisha uhasama lakini juhudi hizo bado zimegonga mwamba na hali bado si shwari.

Inadaiwa kuwa, machafuko hayo yanahusisha makabila mawili ya Kiarabu, ya Misseriya na Awlad Rashed yaliyopo karibu na eneo la Zanglei, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Darfur ya Kati.

Picha: Rais Samia aongoza kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri
Wallace Karia: Ligi Kuu haitasimama