Msanii wa muziki kutoka  nchini Nigeria Ayodeji Ibrahim Balogum ‘Wizkid’ ameachia wimbo wake mpya umnaoenda kwa jina la Deluxe Edition ambao unapatikana katika ya albamu yake ya Made in Lagos.

Wizkid amethibitisha kuachia albamu hiyo mpya leo Agosti 27 kupitia ukurasa wake wa Instagram  kuwa albamu hiyo imeingia sokoni rasmi leo.

Wizkid katika albamu hiyo ameongeza nyimbo mpya nne ambazo ni Anoti, Mood, Steady Pamoja na Essence remix, alifanya na msanii Tems na Justine Bieber kutokea nchini Marekani.

Kabla ya Deluxe Edition, albamu hiyo ilikuwa na nyimbo 14, lakini iliyotoka sasa ina jumla ya nyimbo 18 baada ya kuongezeka nne.

Hata hivyo siku kadhaa zilizopita nyimbo ya Essence ilipata nafasi ya kupanda kwenye chati za Billboard. Pia inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni Duniani kote na Kusababisha mashabiki wa msanii huyo kufikiri kwamba kunauwezekano wa Wizkid kufanya vizuri kwenye tuzo za Billboard msimu ujao.

Wizara ya Afya yapokea vifaa vya milioni 300
Tarehe ya Uchaguzi yatangazwa Jimbo la Ushetu