Mwanamuziki Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu Wizkid kutoka nchini Nigeria, usiku wa kuamkia leo Nov 21, 2021, amefanikiwa kushinda tuzo tatu (3) za AFRIMA kwa mkupuo.

Wizkid alitajwa kwenye kipengele cha msanii bora wa kiume, (Artist of the year), wimbo bora wa mwaka (Song of the year) Essence ft Tems, pamoja na wimbo bora wa kushirikiana (Best Collaboration) Essence.

Wizkid amewapiga chini wasanii kadhaa akiwamo Burna Boy, Diamond  Platnumz, Davido, Sarkodie na wengine. Utolewaji wa tuzo za Afrima 2021, zimefanyika katika Hotel ya Eko, huko Lagos nchini Nigeria.

Dj Sinyorita aibeba Tanzania tuzo za Afrima.
B Dozen awafundisha wasanii njia ya kufanikiwa kimuziki