Muziki wa Tanzania umepiga hodi na kufunguliwa mlango kwa ukarimu wa kipekee na nchi za Afrika Magharibi ambapo wasanii wakubwa wa nchi hizo sasa wanaonenekana kuzitafuta collabo za wabongo.

Wizkid ambaye hivi sasa wimbo wake wa ‘Ojuelegba’ umekuwa wimbo unaopendwa na wasanii wakubwa wa Marekani ambapo Drake aliamua kuingiza verse yake, yeye ameamua kufanya remix ya wimbo wa AY unaoitwa ‘Zigo’.

AY aliweka wazi mpango wa Wizkid wakati anafanya mahojiano katika kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm, ambapo alimuonesha mtangazaji wa kipindi hicho, Lil Ommy ujumbe uliotumwa na mtayarishaji wa nyimbo za Wizkid, Del B.

Ujumbe wa Del B kwa AY ulieleza kuwa wakati huo alikuwa anasikiliza tena ‘Zigo’ na kuimwagia sifa kuanzia mdundo hadi uimbaji. Hivyo, remix ya Zigo kufanywa na Wizkid haiepukiki.

AY na Lil Ommy

AY amepanga kwenda nchini Nigeria kufanya ziara ya vyombo vya habari (media tour) kwa lengo la kutangaza muziki wake. Kutokana na maelezo yake huenda akafanya collabo nyingine na P Square ikiwa ni miaka kadhaa tangu alipofanya collabo na kundi hilo katika wimbo wake ‘Freeze’.

Lowassa Aahidi Makubwa Mbeya, ‘Wahujumu’ Kukiona Cha Moto
“Watanzania Hawahitaji Mabadiliko, Nilizungumza Nao”